You are using an out of date browser. It may not display this or other websites correctly. You should upgrade or use an alternative browser.
Anna Mghwira
MKATABA WA EPA:
Leo Jwakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika wameamua kwa pamoja kusitisha kuweka sahihi mkataba wa EPA hadi Januari mwakani. Awali Kenya na Rwanda walikuwa wamekwisha weka sahihi mikataba hii.
Kwa uamuzi huu unaziweka nchi za ukanda huu katika nafasi salama ya kutafakari na kupima faida na hasara za kusaini mikataba hii.
Tayari Tanzania imeonesha mfano kwa kusita kuingia makbaliano hadi itakapojiridhisha kuhsu faida na hasara za mkataba huu.
Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA Afrika Mashariki na kupata nafasi kujadili mambo haya wakati wakuu wa nchi wakiweka misimamo yao. Umekuwa wakati muafaka kwa matukio haya.
Kwa kusita kusaini na kuzishawishi nchi zingine kusubiri, Tanzania imeonesha njia katika kusimamia mikataba ya aina hii. Nitakuja na taarifa ndefu zaidi lakini kwa hatua hii wenzetu toka nchi jirani wametuheshimu. Tutunze heshima hii na kuendelea kuonesha njia sahihi katika masuala ya diplomasia ya biashara.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.