Ashraj9

AFYA
Afya ni msingi katika maisha ya binadamu.Binadamu yeyote hawezi kufanikiwa katika maisha yake bila kuwa na afya njema na imara.Kwa kiasi kikubwa wote tunategemea sana afya.Kwa kukosa kipaumbele hiko tunashindwa kuziishi ndoto zetu na kufikia malengo.Watu wa zamani walikuwa wanaishi maisha marefu kwa sababu walikuwa na msingi mzuri wa maisha uliopelekea kuwa na afya imara na kudhibiti Maradhi kwa njia ya asili,mfano mzuri tunaona kabisa walikuwa hawatumii vyakula vilivyosindikwa kama sasa. Bali waliishi kwa kula Matunda na mizizi.Hivyo asilimia kubwa waliyaepuka magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ambayo kwa Sasa yamekuwa juu kwa Kasi kubwa.Tumezaliwa tunakua na tunaendelea kuishi bila kujua mtindo wetu wa maisha ndio chanzo kikuu Cha magonjwa sugu ikiwemo saratani, kisukari,moyo na magonjwa ya mfumo wa hewa ambayo yamechochea umasikini katika maisha yetu.
Kuna janga kubwa linalowapata wanandoa.Vijana wengi wa kiume katika rika la balehe wanapitia mihemko ya kimwili hivyo kufanya vitu tofauti. Hilo linaumiza na kuvunja ndoa nyingi kila kukicha. Ukosefu wa nguvu za kiume limekuwa janga duniani.Ngoja nitolee mfano ukichukua muhindi vile jinsi ulivyo Ile shepu ndivyo maisha ya kijana yalivyo ukiaangalia na kuchukua ule muhindi kule juu na chini katika kikonyo radha ni tofauti maana yake ni nini? Ni kwamba kijana ukiwa balehe kuanzia miaka 18 Hadi 25 uwezo wako wa kuzalisha ni mkubwa mno pale kiafya mbegu zako zina nguvu mno ila sasa kijana unajihusisha na kujichua,tutambue kuwa mtu anapojichua kile kitendo anarudisha misuli nyuma na kwa hali hiyo lazima misuli isinyae kwa sababu mikono ni migumu na maumbile yako ni laini kiuongo lazime kisinyae hivyo kadri umri unavyokua seli zinazidi kukua na kupelekea misuli kushindwa kufanya kazi na matokeo yake ni kulegea kwa kiungo mwisho watu wanalalamika kwamba ,wanakosa hamu ya tendo la ndoa kumbe kile kipindi Cha ujana kipindi ambacho wananguvu walikuwa wanafanya vitu vya ajabu sasa inapofikia miaka 45 pale uwezo wa kuzalisha unakuwa mdogo zile mbegu zilizo na nguvu umezimwaga chooni kwa sababu tu ya kujichua na mbaya zaidi matumizi ya dawa za kusisimua unatumia pia sasa matokeo yake ndio upungufu wa nguvu za kiume umekuwa tishio kubwa na kupelekea ndoa nyingi kuvunjika.
Wanawake pia kumekuwa na janga la saratani na kupelekea vifo vingi vya kinamama uthibitisho nenda ocean road kina mama idadi kubwa ya walioathirika wanawake, walio katika umri mdogo kabisa . Mfumo wa maisha tunayoishi hususani katika njia za uzazi wa mpango ndio chanzo.Mwanamama unapotoka kwenda kituo Cha afya unapohitaji huduma juu ya uzazi wa mpango utapewa ila hawakwambii madhara ya njia hiyo kwasababu chochote utakachotumia kinapoingia katika mwili kitaenda kufanya kazi kuzuia ujauzito hivyo lazima kiharibu kitu ndani ya mfumo wako wa uzazi Leo hii mtu anaenda kutoa ujauzito kwa njia zisizo sahihi ananunua vidonge anatumia kuharibu ule ujauzito kwa viambata sumu venye kemikali bila kujua ni hatari kiafya hivyo ndio chanzo cha saratani kwasababu unakuta binti mdogo hajajifungua mtoto hata mmoja lakini anapata kansa. hivyo yote hiyo ni kwasababu anatumia vitu vyenye sumu katika mwili wake kwahyo wanapofika kituo Cha afya waelekezwe njia sahihi zisizo na madhara katika mwili wake kama matumizi ya kalenda.
Mda mwingine kushamiri kwa utandawazi kumepelekea kutokea kwa vitu ambavyo vinazalisha sumu katika miili yetu ukitofautisha na wenzetu walivyokuwa wanaishi zamani.Mfano katika swala Zima la kilimo kuna baadhi ya wakulima wametenga kabisa mazao ya kilimo kwa ajili ya matumizi binafsi na biashara asilimia kubwa kwakuwa ana uhitaji wa pesa kwa haraka mbolea za kupandikiza,kukuzia na kuua wadudu zinatumika katika mazao hivyo hata ukila ugali wa Dona unakula ile ambayo imelimwa katika mbolea na baada ya kupata madini ambayo yangefonzwa na mahindi ardhini unapata sumu ambazo mahindi yalifyonza chini ya ardhi yani zile mbolea na kwa wanaonunua dona madukani sumu nyingime ni zile ambazo zilitumika kuhifadhi mahindi yasiliwe na wadudu .Kumbuka mfanyabiashara hana muda wa kuosha magunia elfu moja ili kusaga unga na sasa hivi hadi mboga za majani zinawekwa mbolea za chumvi wakati zamani ni samadi tu kwahiyo tunaona kabisa mtindo wa maisha ndo changamoto katika Afya zetu.Mazao mengi sana siku hizi yamechakachuluwa yani mazao ya mwendokasi kwa muda mfupi kuanzia matunda,mbogamboga na mengineyo kwahiyo hayana virutubisho vya asili Mungu alituwekea hata radha zimebadilika.
Pia katika kilimo Kuna mashine za kukoboa yani utakuta mchele unakobolewa wakati zamani mpunga wazee wetu walikuwa wanatumia vinu kutwanga kwa sababu kufanya hivyo inasaidia ile leya ya juu yenye mafuta haiondoki kwanza ndio Nafaka kamili ambayo inahitajika katika miili ya binadamu.
Watanzania tunaweza kulijenga daraja la mafanikio na maono yetu ni ya mbali. Ushauri wangu ni kwamba kubadilisha mfumo au mtindo wa maisha tunayoishi Kuna faida kubwa sana Ili kuepusha Maradhi sugu na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ambayo kwa sasa ni tishio kubwa katika Afya kwani afya ni utajiri siku zote ukiwa na afya bora hata uwezo wa kufikiri ni mkubwa pia hatuchoki hivyo chachu ya maendeleo ndio maana tunaambiwa tutunze mazingira yawe safi kwa viumbe vyote binadamu na wanyama.
Tukae tukijua Afya ni mafanikio.Tunapoteza pambano hili sisi wenyewe maradhi mengi sugu yataongezeka duniani katika Karne ya sasa. Tunaona matokeo watu wengi Sasa hivi wanapoteza maisha na chanzo kikuu ni moja ya Maradhi sugu amabayo tumeyataja kwani tumepoteza watu mahiri na mashughuri ambao wangechochea maendeleo kiuchumi.Tunashindwa kudhibiti uzito ,kazi zetu nyingi za kuushughulisha mwili na kikubwa zaidi mlo wetu hauna virutubisho vya chakula ambavyo labda vinapatikana katika mlo kamili kama vile nafaka kamili na matunda Pamoja na mbogamboga.
Vilivyotajwa hapo ndio lishe bora kwangu na kwako kama binadamu mwili ndo unahitaji katika mtindo wetu wa maisha.Ikitokea tunavipata basi daraja letu la mafanikio halitakuwa na changamoto kwani tutafanya kazi kwa juhudi na ufanisi kwasababu tuna afya njema.Tumepatwa na janga la Korona tumeona jinsi gani Kinga zetu zilivyo chini na kupelekea vifo vingi.Sasa swali kwangu na kwako je tunaziishi ndoto zetu?katika maisha yetu ya Kila siku tukikumbwa na matatizo tunaamini pombe na sigara ndio mwisho wa matatizo yetu au ndio ukomo wa shida sasa tumewai kujiuliza ni muhimu kwa afya ?
Hakuna marefu yasiyo na ncha hata moyo pia unachoka mwisho wa siku tunazidisha viambata sumu mwilini na hapo ndipo tunapata matokeo kuwa mtindo wetu wa maisha ndio chanzo kikuu Cha maradhi sugu yanayotukwamisha kuleta maendeleo.
Birthday
Jul 8, 1999 (Age: 26)
Location
Dar es salaam
Gender
Female
Occupation
Student

Trophies

  1. 25

    Somebody Likes You

    Somebody out there liked one of your messages. Keep posting like that for more!
  2. 20

    First Message

    Post a message somewhere on the site to receive this.
Back
Top Bottom