yesse lambert

Wapendwa naamini hamjambo kabisa.
Napenda kuwajulisha kuwa tangu nimewajuza kuhusu program ya Maarifa ya Kazi, wale waliojitokeza na kuanza kupata huduma hii wanaendelea vizuri.
Kwa ujumla huduma hii inatolewa kwa njia ya masafa. Unajifunz hapo ulipo na unafanya kazi zako hapo ulipo. Hakuna haja ya kutumia mda wako kusafiri, kuachana na familia yako, kusitisha shughuli zako zingine n.k
Kwa ufupi ni kwamba mafunzo yenyewe yanakuwezesha kufanya yafuatayo:-
1. Kuzalisha chakula cha mifugo aina mbali mbali maarufu kama hydroponics Green Fodder
2. Kuandaa bustani za mbogamboga nyumbani kwako pasipo kuwa na shamba.
3. Kuandaa viua wadudu kwa njia ya asili.
4. Kuandaa mbolea za maji zisizokuwa na madhara kwenye mimea na mifugo.

Mafunzo hayo yatafungua fursa nyingi kwa vijana walioko katika eneo lako sambamba na kukufungulia fursa nyingine wewe mwenyewe utakayekuwa umejifunza.
Nakaribisha swali lolote lile kwa yule ambaye atakuwa amesoma na hajanielewa.
Pia nichukue fursa hii kuwashukuru wataalam wa mifugo toka Mwabuki walionitembelea shambani kuja kuangalia namna program inavyoendelea. Naamini zipo taasisi nyingine zinazoweza kushirikiana nami katika shughuli hii ila hawajapata nafasi ya kujua nini kinaendelea.
Watanzania tumekuwa tukishangaa ni kwa nini mayai toka Uganda yanauzwa kwetu kwa bei ya chini tofauti na ya kwetu. Siri ndo hiyo, wao walianza mapema kutumia teknolojia hii katika malisho ya kuku na wanyama wengine.
Niko tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi za kiserikali, zisizo za kiserikali na watu binafsi kuhakikisha jamii ya watanzania inatokana na mawazo mgando ya kuendelea na ufugaji wa kizamani.
Wale members mlionitafuta na kunishirikisha katika hili nawashukuruni sana, tuendeleeni kuwajuza na wengine.
'JF zaidi ni zaidi ya Chuo
Birthday
Jan 1, 1999 (Age: 27)
Gender
Male

Trophies

  1. 50

    Keeps Coming Back

    30 messages posted. You must like it here!
  2. 25

    Somebody Likes You

    Somebody out there liked one of your messages. Keep posting like that for more!
  3. 20

    First Message

    Post a message somewhere on the site to receive this.
Back
Top Bottom