Ahmed Rajab na Rais Mstaafu Jenerali Ibrahim Babangida
KAMA kuna mtawala wa kijeshi aliyewaweza Wanigeria basi alikuwa Ibrahim Badamasi Babangida (IBB) au “Maradona”, kwa umaarufu wake wa mitaani. Si bure kwamba alibandikwa lakabu hiyo ya jina la mchezaji soka maarufu wa zamani wa Argentina...