Sheria imeweka kinga maalum za msingi ili kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa ya staha na heshima kwa kukataza ajira ya mtoto, ajira ya shuruti na kupiga marufuku ubaguzi katika ajira. Makatazo haya yanawahusu pia, Jeshi la Wananachi wa Tanzania, Polisi, Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa...