Mtunzi: RamaB.
Hivi hawa matajiri, walifanya kazi gani?
Kuondoa ufakiri, wakawa mamilioni.
Nipeni yao siri, iniingie kichwani.
Kuchuma najitahidi, sina bahati mwenzenu.
Nikalikamata jembe, panga na shoka begani.
Nikautoa uzembe, mpunga panda kondeni.
Ukajaliwa na ng’ombe, nikabaki kichwa...