Bongo Flava ni jina Mbadala la muziki wa Hip hop ya Tanzania. Mtindo huu ulianzishwa kwenye miaka ya 1990, hasa ukiwa kama mwigo au utokanaji wa hip hop kutoka Marekani, ikiwa na ongezeko la athira ya muziki wa reggae, R&B, afrobeat, dancehall, na mitindo ya asili ya Kitanzania kama vile taarab...