“Kwenye suala la Ngorongoro, ilitakiwa twende huko kesho Ijumaa kwenye Mkutano, tuliomba mikutano mitatu, Makalla (Mwenezi wa CCM Taifa) alivyoona akatoa ratiba ya mkutano, nikamwambia Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini kuwa Makalla ameitoa hiyo ratiba makusudi, hawa wana mpango wa kutunyima...
Jeshi la Polisi nchini limezuia mikutano ya hadhara ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyopangwa kufanyika wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha kuanzia Agosti 29.2024 hadi Septemba 15.2024, mikutano iliyotarajiwa kuongozwa na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Gabriel Makala...