Kwa wanaofuatilia siasa za Mozambique, hali ni mbaya kwa chama tawala cha Frelimo pamoja na serikali iliyoko madarakani. Baada ya uchaguzi kuisha na serikali kujitangaza kushinda kwa wastani wa asilimia sabini, wananchi wameikata, wakiongozwa na kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane...