Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali iko mbioni kupeleka Bungeni pendekezo la chanzo kipya cha mapato kitakachowezesha Wizara ya Ujenzi kupata fedha itakayotumika kusaidia masuala ya dharura.
Dkt. Mwigulu amesema hayo wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara...