"Nitoe wito kwa OCD Misungwi, nitoe wito kwa RPC Mwanza, nitoe wito kwa Waziri wa mambo ya ndani, na nitoe wito kwa anayefanya kazi ya kuteua hao wote, Amiri jeshi mkuu ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nitoe wito kwamba maisha na uhai wa mtu mmoja unafaa kuwa na thamani kubw...