Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linamshikilia Christina Shiriri (43) kwa jina maarufu Manka, mfanyabiashara na mkazi wa Usagara wilaya ya Misungwi kwa kosa la kumfanyia ukatili mfanyakazi wake wa ndani Grace Joseph (17), mkazi wa Kijiji cha Nyalwigo wilaya ya Misungwi kwa kummwagia mafuta ya taa...