Watoto huzaliwa wakiwa na uwezo wa kunyonya bila kufundishwa (sucking reflex). Kitendo hiki ni muhimu sana kwasababu ndiyo njia pekee ya kumpatia chakula mtoto mdogo. Sayansi imeonesha kwamba mtoto huanza kunyonya (vidole) tangu akiwa tumboni kwa mama, hii inaonekana kupitia picha za ultrasound...