Katika ukanda mmoja wa Kusini wa Bara la Asia, palikuwa na mfalme mmoja ambae alitawala himaya yake kwa weledi na ufanisi mkubwa mno. Mfalme huyo alikuwa akipenda sana haki na utiifu mno, kiasi kwamba aliwaadhibu vikali mno wale wote walioenda kinyume na sheria na taratibu za himaya yake...