dawasa mbezi beach

No Wikipedia entry exists for this tag
  1. P

    KERO Krismasi imeisha tumerudi kwenye mgao wa maji! Kama tulipata huduma vizuri Krismasi ina maana mgao huu ni makusudi?

    Wakuu, Msemaji wa Mbezi Beach nimekuja kwa mara nyingine. Kwa Mbezi maji yanakatika kila siku na wakati mwingine inaweza kuwa siku mbili na zaidi. Muda wa kukatika ni kuanzia jioni (kwenye saa kumi hivi) mpaka kesho yake kwenye saa nne au tano hivi. Kwahiyo kwa siku mara mnyingi maji hutoka...
  2. P

    KERO Waziri Aweso kama kuna mgao wa maji Dar mtuambie, maji unayojitapa yapo ya kutosha hatuyaoni mtaani

    Wakuu, Nakuja kwenu Afisa Maji wa kujiteua mwenyewe kwa wakazi wa Mbezi Beach na Dar kwa ujumla. Kiukweli Dar kuna upungufu mkubwa wa maji, yaani kadri siku zinazovyoenda hali inazidi kuwa mbaya. Kama sisi wa Mbezi Beach sasa hivi ni kupata maji kwa masaa mamache yanasepa, ukitoa taarifa...
  3. P

     Baada ya kelele za kutosha JF hatimaye maji yaanza kutoka na presha inaridhisha, maeneo mengine bado hayajifika muwafikie na wao

    Wakuu, Pongezi sana JamiiForums kwa kutupazia sauti mpaka maji yameanza kutoka na presha ipo vizuri tofauti na siku tatu za nyuma kabla ya maji kukata kukabisa. Nimeona Waziri amekuja kujibu na kusema kati ya sehemu kuna huduma ya uhakika ya maji ni Mbezi Beach! Huu ni uongo mkubwa Wizara ya...
  4. P

    KERO Siku ya 4 Mbezi Beach hatuna maji, mpaka sasa hatupewi majibu ya kuridhisha hali inazidi kuwa tete. Si mje mng'oe na hizi mita zenu tujue moja

    Wakuu, Msione kila siku napiga kelele mkadhani nazingua, leo naweka baadhi ya screenshot muone majibu ya DAWASA ya kipuuzi na wananchi tunavyolilia huduma utafikiri tunaipata bure! Pia soma: √ - Waziri Aweso: Tatizo la Maji Mbezi Beach Mkoani Dar Es Salaam limeisha. Kulitokea Hitilafu Kweli...
  5. P

    KERO DAWASA Mbezi Beach mnatuona manyani tu, Aweso pita na huku tafadhali kuna shida pahala inahitaji kunyooshwa

    Wakuu, Nishachoka kuja kulalamikia maji hapa, mnatufanya kama watoto tunapewa pipi tumun'unye halafu mnatupokonya. Yaani kama vile sasa hivi tupo kwenye mgao, na maji bado yana harufu mbaya, ukiwatafuta majibu ni yale yale, maji yameruhusiwa yatatoka! Ahhh Wizara ya Maji embu pitia huko nyuma...
  6. P

    KERO Maji yanatoka Mbezi Beach lakini presha ni ndogo sana hata kama una tenki la akiba ni kazi bure, maeneo mengine Dar hali ikoje?

    Wakuu kwema, Nilikuja na uzi hapa baada ya kukosa maji karibu siku 5 bila taarifa yoyote, baada ya malalamiko kupelekwa Insta maji yakaanza kutoka, lakini toka yaanze kutoka presha ni ile ile, ndogo sana. Mpaka leo hii maji yanatoka kidogo kidogo sana kiasi kwamba hata kama mtu una tenki la...
  7. P

     Hatimaye maji yameanza kutoka Mbezi Beach kwa Zena, JF mbarikiwe

    Wakuu, kumbe vitu vikiruka kupitia JF mambo yanaenda eeeh? Baada ya JF kurusha maji yamerejea, hapa ndio pa kuleta kero zetu Wakuu. Tukaoge vizuri na kuosha vyombo vichafu vya siku mbili. JF iishi milele🔥🔥🔥 Pia soma: KERO - Mbezi Beach kwa Zena hatuna maji siku ya 3 leo tatizo ni nini?
  8. Mkalukungone mwamba

    KERO DAWASA kwanini mmeshindwa kutoa majibu kwa Wakazi wa Mbezi Beach maji ya bomba kutoka machafu kwa muda sasa

    DAWASA leo katika mkutano na waandishi wa habari mmeulizwa kuhusu tatizo la kutoka maji ya bomba yakiwa machafu kwa baadhi ya wakazi wa Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam. Hii inamaanisha nini kwa sisi wakazi wa maeneo haya? Maji ya bomba ni machafu yanayotoka katika maeneo yetu yanazidi...
  9. P

    KERO Maji ya bomba yanazidi kuwa machafu kadri siku zinavyokwenda, DAWASA maji haya yana usalama kweli?

    Wakuu kwema, Maji yamekuwa yakitoka machafu kwa muda sasa, sasa hivi hali inazidi kuwa mbaya, maji ni machafu sana mpaka yanatia mashaka kwenye usalama wake, mbali na kuwa machafu kama hivi yana harufu mbaya pia kama vile kuna kitu kimeoza, japokuwa siyo strong sana lakini unaipata. Kama maji...
  10. P

    KERO DAWASA mna nini na wakazi wa Mbezi Beach? Hatuna maji siku ya 3 sasa

    Wakuu salam, Wakazi wa Mbezi Beach hatuna maji ni siku ya tatu sasa, kuna nini? Au kuna matengenezo yalitangazwa na yamenipita? Maana sijasikia popote, hata kama kuna matengenezo ndio siku tatu jamani? Mnafikiri tunaishije? Halafu maji hayajaacha kuwa na machafu/vumbi! Sasa vumbi kwenye maji...
  11. A

    KERO Wakazi wa Mbezi Beach tunapata maji ya bomba machafu, na yana harufu mbaya. Mlipuko wa magonjwa unakuja

    Habari JF, Ni wiki na zaidi sasa maji yamekuwa yakitoka machafu hivi na wakati mwingine huwa machafu zaidi na yenye harufu mbaya. Niliuliza kwa mjumbe maana ni jirani yangu kama anakutana na tatizo hilo nikitaka kufahamu huenda ni mimi tu, naye akasema yapo hivyo na kwake pia (maji yalikatika...
Back
Top Bottom