Wakuu kwema?
Leo ni siku ya tatu Mbezi Beach kwa Zena mtaa wa Mbezi Beach B hatuna maji.
Hakuna taarifa yoyote tuliyopewa juu ya mgao huu, mnafikiri tuko kwenye mazingira gani DAWASA?
Ni kama mmetuamulia wakazi wa huku, haipiti muda lazima tupate changamoto ya kutokuwa na maji kwa siku...
Wananchi wa Mbezi Juu, Baraza la Mitihani wanalalamika sasa ni mwezi hawajaona maji, inabidi watafute maji mbali kwa magari.
Kwa gharama hii ya maisha hamuoni ni mzigo mwingine?
Kama Dar inakuwa hivi huko vijijini je?
Kwa sasa maji hayana ratiba maalumu ila hapo mwanzo tuliaminishwa kuwa kwa sasa hapata kuwa na crises ya maji.
Maeneo mbalimbali ya Mbezi maji ni ya shida sana, Serikali iko kimyaa, kinachoshabgaza hivi serikali za mitaa kazi yake nini kama watu wanateseka na maji wiki 3 bila maji watu...