Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru China kwa kufikia hatua za mwisho za kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR ambao unaendelea hivi sasa kwa kipande cha tano cha kuanzia Mwanza hadi Isaka na kuahidi kuyafanyia kazi maombi mengine ya kipande cha sita kinachoanzia Tabora...