ega

eGA
Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019. Ni taasisi yenye Ithibati wa Viwango vya Ubora (ISO 9001: 2015) katika kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao pamoja na kuhimiza utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao kwa taasisi za umma.

Mamlaka ya Serikali Mtandao ni taasisi iliyoirithi Wakala ya Serikali Mtandao iliyoundwa Aprili 2012 kwa Sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 Sura ya 245 ya mwaka 1997 yenye jukumu na Mamlaka ya Kuratibu, Kusimamia na Kukuza Jitihada za Serikali Mtandao nchini Tanzania.

Kabla ya kuanzishwa Wakala ya Serikali Mtandao, matumizi ya TEHAMA Serikalini yalikuwa yanaratibiwa na kusimamiwa na Idara ya Usimamizi wa Mifumo (DMIS) iliyopo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambayo kwa sasa ni Idara ya Huduma za TEHAMA Serikalini (DICTS).

Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019 imeainisha majukumu na mamlaka yanayoiongoza Mamlaka ya Serikali Mtandao katika utekelezaji wa Serikali Mtandao nchini Tanzania.
  1. olimpio

    Kutaka kuiua eGA na kuipa tender NMB za TEHAMA inaaiwa kumtoa Nape

    Mwaka mmoja na miezi yakutosha niliwahi kuwajulisha juu ya njama za kutaka kuua eGA, Watu kadhaa inadaiwa walikua nyuma ya carpet wakiandaa mikakati hio. Hivi karibuni inadaiwa watu hao walifikia 98% kuiua eGA, wazalendo wa Makumbusho wakaokoa jahazi dakika za jioni sana (Hongera sana kwao)...
  2. olimpio

    eGA inauawa rasmi?

    Sio jambo rahisi sana kujitoa mhanga kuyasema haya, na kipekee nimshukuru Maxence Melo kwa kuweka jukwaa hili; linasaidia sana kupashana habari. Niwafungue macho kidogo: eGA kupelekwa wizara ya TEHAMA ni jambo lililojaa siasa kubwa sana na uhalifu mkubwa kwa nchi, ni jambo ambalo wametengenezwa...
  3. olimpio

    e-GA inahujumiwa

    Miezi takribani sita imepita niliandika juu ya njama za viongozi waandamizi wa serikali kuihujumu mamlaka ya serikal mtandao(e-GA). Mipango ya e-GA kuzuiwa kufanya majukumu ya uundaji wa mifumo ya serikali ili waandamizi watafute kampuni binafsi kufanya hayo imeanza kufanikiwa. Leo Wizara ya...
  4. olimpio

    DOKEZO Wanasiasa na mipango ovu ya kuiua eGA

    E-GA ni taasisi inayoratibu serikali mtandao, ni taasisi ambayo inajenga mifumo karibu mingi sana inayotumika na serikali. Serikali imeokoa pesa nyingi sana kutoka nje ya nchi na imetoa ajira kwa wazawa. Zaidi sana taarifa na usiri ama unyeti wa taarifa za serikali umeongezeka baada ya mifumo...
Back
Top Bottom