Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga ameeleza kuwa Jeshi la Polisi linamshikilia Elias Obadia Mwaimse [30] Mkazi wa Mikoroshini Wilaya ya Kyela kwa tuhuma ya kuvunja ofisi mchana na kuiba silaha moja aina ya Short Gun yenye namba T.26444, TZ CAR NA.55089 na risasi zake 17...