Rafiki yangu mpendwa,
Kuna watu huwa wanabana sana matumizi, wanakuwa na ubahili mkubwa kwenye fedha zao, lakini bado wanashindwa kujenga utajiri.
Watu hao huwa wanajisifia mbele ya wengine jinsi ambavyo hawana matumizi mabaya na ya anasa. Wamekuwa wanawaona wale wanaokuwa na matumizi makubwa...