Nimepita Mbagala wiki hii nikielekea kwenye Shamba langu Mkuranga, Hakika Mbagala ni Nchi nyingine kabisa, Utaratibu wao wa kuishi ni tofauti kabisa na Utaratibu wa Tanzania.
Wamachinga wamepanga bidhaa kuanzia kwenye milango ya maduka ya watu hadi katikati ya Barabara bila wasiwasi wowote...
Bila shaka huyu ni kigogo mzito sana, anajenga frem kwenye hifadhi ya barabara, ndani ya kituo cha mwendokasi Mbagala, kibali amepata wapi? Ilikuja Tanroad ikasimamisha ujenzi na kupiga X jamaa akafuta kwenye x za kijivu ujenzi unaendelea, wakaja tena wakarudia kupiga X bado mafundi wanapaua...