Sipajui sana Geita, lakini napafahamu, alau kidogo. Habari zake zimevuma ndani na nje ya Tanzania, hasa kwa shughuli za "uvunaji" dhahabu!
Hivi karibuni, nimesimuliwa kuwa baada ya Mzungu mmoja huko ughaibuni kukutana na dhahabu iliyodaiwa kuwa ilichimbwa na kampuni ya Geita Gold Mine (GGM)...