Takribani miezi 10 ama 11 hivi nilikuwa sijagusa mpira, siku hiyo mwili wangu unatamani mpira kuliko chochote, hata ule mchezo wa mguu bara mguu pwani siutamani kama ambavyo nimeamka na tamaa ya kucheza mpira, akili yangu haiwazi mengine kikamilifu ni mpira tu, kila mara najiona kama uwanjani...