Siku hizi ukikutana na mtu ambae hukumchangia harusi yake basi utakuta hakuchangamkii kama zamani.
Jamani sisi sio fake friends ni hali ngumu jamani mtusamehe bure
Hii app ya Whatsapp sioni faida yake kabisaaa imegeuka kausha damu kwangu, imagine nina group tano za michango ya harusi na zote zinadai 50K kwenda juu. Na bado sijui kama kutakucha bila kuongezwa kwenye group jingine.
Yaani kila siku unaungwa kwenye magroup mpya za harusi, watu hata huwajui...