Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewakuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, na wenzake wawili hivyo wanatakiwa kuanza kujitetea kesho Ijumaa Agosti 13, 2021.
Mbali na Ole Sabaya, washtakiwa wengine katika shauri hilo la jinai namba 105 ni Sylvester Nyegu (26)...