Napenda kutoa malalamiko yangu makali na kero kuhusu kucheleweshwa kwa malipo ya fidia kwa ardhi tuliyotoa KIPUNGUNI kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa serikali. Taarifa ya tathmini ya ardhi ilifanywa tangu jana, na hata miaka ya nyuma (1997), lakini hadi leo hatujaona malipo yoyote...
Nilimsikia Mbuge wa Segerea akitoa notisi ya kushikilia shilingi ya Waziri wa Uchukuzi kuhusu malipo ya fidia Kipunguni A lakini ghafra ikawa kimya je kulikoni na wewe unatusaliti Mungu yupo naamini atatulipa tu. Asanteni sana kwa kututesa
Ni aibu iliyoje kwa serikali kushindwa kulipa fidia Kipunguni kwa kipindi cha miaka 27 na zaidi. Je, mwenye kustahili kuwajibika Waziri wa fedha, Uchukuzi, TAA au Rais na mwenyekiti wa CCM, tuambiwe.
Waziri Mkuu ingilia kati kuna mchezo mchafu. Mbunge Kamoli amelisemea sana sasa joma na iwe...
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kamoli akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2024/25 leo Mei, 6, 2024 amesema ikiwa suala la fidia ya wananchi wa Kipunguni halitapatiwa maelezo ya kutosha, basi atashika shilingi na hataachia.
Amesema suala hilo limechukua muda...
Mheshimiwa Rais mama yetu mpendwa. Wakazi wa Kipunguni Dar salaam ambao tuliteseka Zaid ya miaka 20 mwaka huu tumefanyiwa tathimini ya majengo na ardhi. Tunasubiri malipo.
Lakini tunaona siasa zimeanza maana mpaka Sasa bado hatujajua lini tutalipwa. Ingawa mmbunge wetu Segerea Bona Kimori...