Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwachukulia hatua watumishi wote waliobainika kusababisha changamoto kwenye miradi inayotekelezwa Sumbawanga akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa manispaa hiyo Jacob Mtalitinya...