Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameshusha neema kwa wananchi wa Kilosa kwa uamuzi wa kufuta jumla ya mashamba 11 yenye ukubwa wa ekari 24,119 katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro na kugawiwa kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za kilimo, ufugaji na uwekezaji...