1. Ni bei ya Samaki kilo moja
2.Ni bei ya kuku wa nyama mmoja na chenchi inabaki
3.Unatoa mikeka 10 ya buku kwa mhindi
4. Sukari kilo 3
5. Dona kilo 4
6. Mchele super kilo 4
7. Maziwa ya Ng'ombe lita 4
8. Soda take away 10
9. Luku unit 28
10. Tofali za ujenzi 10
Hivi wanaume wenzangu mnaohonga nyumba Mpaka magari Nyoyo zenu zipoje? Maana mimi nimejaribu ELFU KUMI tu yaani hapa natetemeka mwili mzima jasho, halikauki yani nahisi kuzimia zimia😂😂
Sina haja ya salamu ila nataka tu kuwakumbusha ndugu zangu wa kiume ukiona unatumia nguvu kubwa ya kifedha kuendesha mahusiano jua tu huyo mwanamke hakupendi.
Mahusiano sio magumu wala sio ghali kiasi hicho iwapo utapata mtu sahihi.
Naishia hapa naomba kuwasilisha.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.