Mtu anakuja kwako analia, kilio cha msibani. Anapiga magoti umkopeshe pesa. Unamkopesha kwa moyo safi kabisa. Anaondoka kwa shangwe utafikiri bwana arusi kaoa. Muda mliopatana wa kulipa deni ukifika, ghafla anapatwa na "ugonjwa wa kusahau kulipa madeni."
Ugonjwa usiotibiwa hospitali, ambao dawa...