Maelfu ya Waisraeli wamekusanyika nje ya bunge jijini Jerusalem wakishinikiza Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu ajiuzulu.
Aidha, waandamanaji wanataka kuitishwa uchaguzi mpya mapema, na Serikali ifikie makubaliano ya kuachiwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas tangu kuanza kwa mapigano Oktoba 7...