Mahakama ya juu nchini Uganda imeamuru kuwa kesi zote zinazowahusu raia ambazo zilikuwa zikisikilizwa katika mahakama za kijeshi zisitishwe mara moja na kuhamishiwa katika mahakama za kawaida.
Uamuzi huo umetolewa na jopo la majaji saba, likiongozwa na Jaji Mkuu Alfonse Owing Dollo, ambao...