Watumiaji wa intaneti nchini Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa intaneti huku watoa huduma kote Afrika Mashariki wakikiri kumekuwa na tatizo.
Wamesema wanajitahidi kurekebisha tatizo hilo.
Huduma hiyo ilikumbwa na hitilafu katika nyaya za chini ya bahari...