Sina uzoefu mwingi wa matumizi ya mitandao ya kijamii, bado mshamba kiasi, na neno KARMA nimelipata humuhumu jamii forums. Katika kutafutatafuta maana ya KARMA kwa kutumia kamusi za humuhumu mitandaoni nikaelewa kuwa KARMA ni malipo anayoyapata mtu kutokana na maovu aliyowafanyia wengine...