Jumla ya madaktari bingwa 49 waliotumwa na Rais Samia wamewasili mkoani Arusha, wakipokelewa na uongozi wa mkoa huo kwa lengo la kushiriki kambi ya matibabu ya siku sita itakayohusisha wilaya zote saba za mkoa huo. Madaktari hao wametakiwa kutoa huduma kwa moyo wa huruma na kujituma kwa wananchi...