Mfumo wa Elimu tulionao hapa Afrika hatukuutengeneza sisi wenyewe bali maadui zetu, hivyo kamwe usitegemee adui yako akupe elimu nzuri. Akupe elimu nzuri ili umpindue? Wazungu walipokuja kwa mara ya kwanza hapa Afrika, walitukuta tuna mfumo wa elimu wa ujuzi na badala yake wakauua na kutupa...