Wakuu,
Zile mia mia na hela za michango ya mitihani na nyingine ambazo hazina maelezo yanayoeleweka toka kwa mkuu wa wilaya au mkurugenzi mjue ni usumbufu kwa wazazi.
Hapo mzazi akigoma kulipa mwanafunzi anachapwa au anaambiwa asiende shuleni, haya matamko ya kisiasa yanaharibu sana elimu...
Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu amesema sera ya elimu bure inayopigiwa kelele na Serikali ya CCM ni ulaghai mtupu. Haitekelezeki kwa ufanisi kiasi cha kurejesha tena michango lukuki kwa wazazi.
“Wazazi wanachangishwa fedha kwa ajili ya mitihani, vitabu, chakula, walinzi, ukamilishaji wa...