Wakuu,
Serikali ya mkoa wa Lindi imesema kuwa ndani ya Mkoa wa Lindi watoto kati ya miaka 10 hadi 19 wakiwa na jumla ya watoto 7,840 wamepata Mimba na kukatisha masomo jambo ambalo halikubaliki katika jamii na Serikali kwa ujumla.
Soma pia: Changamoto ya Mimba za Utotoni, Katavi, Watoto 50 wa...
https://feminahip.or.tz/
FEMINA HIP mmepotelea wapi ndugu zetu? Zamani mlitoa elimu kwa vijana juu ya maambukizi ya magonjwa ya ngono, mimba za utotoni nakadhalika. Vijana wengi tulivutiwa sana na Magazine za Femina Hip kwasababu tulifahamu njia zote mbaya za kutuingiza kwenye vishawishi vibaya...
Takwimu za Mimba za Utotoni na Ripoti za Matukio ya Ukatili Mkoani Katavi kwa Mwaka 2024
Muda: Januari – Oktoba 2024
Waliotoa taarifa za kufanyiwa ukatili
Wanawake - 2,740
Watoto (Wasichana) - 614
Wanaume - 981
Watoto - 231
Mimba za Utotoni
Watoto (Miaka 10 - 14) - 50
Watoto (Miaka 15 - 19) -...
Kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa Kijiji Cha Kilambo ambaye ni Mwanafunzi wa kidato Cha nne katika shule ya Sekondari Ikimba Wilayani Kyela amehukumiwa kifungo Cha nje Cha miezi 12 pamoja na faini ya kiasi Cha shilingi laki mbili Kwa kosa la kubaka na kumpa Mimba Mwanafunzi...
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza amefanya Ziara ya Kata kwa Kata huku akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa Kata ya Shiwinga iliyopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Mhe. Juliana Daniel Shonza amesema kuwa lengo la ziara yake ni kuelezea Utekelezaji wa Ilani ya...
TANZANIA TUITAKAYO BAADA YA MIAKA MITANO NI KUTOKEMEZA MIMBA Z A UTOTONI NDOA ZA UTOTONI KWA KUANZISHA NA KUIMARISHA MITANDAO YA KIJAMII NA KISHERIA AMBAYO INASHUGHULIKIA UKATILI WA KIJINSIA, KUFUTA HAKI FULANI ZA KIJAMII AU KISHERIA KWA WAHALIFU WA UKATILI WA KIJINSIA, KAMA VILE HAKI YA KUWANIA...
WATOTO WA KIKE WANAOKOSA MALEZI YA BABA WAPO HATARINI KUANZA MATENDO YA NDOA KATIKA UMRI MDOGO NA KUPELEKEA MIMBA ZA UTOTONI
Na Comrade Ally Maftah
KING OF ALL SOCIAL MEDIA
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali inaonyesha kwamba mtoto anayekosa malezi ya baba anakuwa hatarini kupata mimba za utotoni...
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema katika Mikoa ya Dar es salaam, Njombe na Ruvuma viwango vya mimba za utotoni vimeongezeka, huku mapambano ya kupunguza idadi ya mimba hizo yakirudi nyuma ambapo amewataka Wazazi waendelee kuwalinda Watoto wetu dhidi ya mimba za utotoni.
Rais...
Tuondoea umasikini wa Vipato ili kumaliza tatizo la Ndoa za utotoni na wanafunzi kupewa Mimba.
Ukijaribu Kusoma Historia ya wazungu hasa maisha yao ya miaka ya 1800 huko hadi 1930 huko utagundua kwamba haya yanayo tokea huku kwetu sasa pia na kwao yalikuwepo, Wazungu walikuwa na Ndoa za...
SERIKALI KUSHIRIKIANA NA TAMWA KATIKA MASUALA YA AFYA YA UZAZI MAMA NA MTOTO.
Na. WAF - Dar es Salaam
Serikali kupitia Wizara ya Afya imedhamiria kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) katika kupambana na kutoa elimu juu ya masuala ya Afya ya Uzazi Mama na...
Karibuni katika kuchangia mawazo ili kuweza kupata mbinu zitakazo wezesha kumnusuru mtoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni na ukatili wa kingono,mara nyingi naweza sema kuwa serikali imekuwa nyuma sana katika kuhakikisha kuwa inazuia na inaweka mazingira ambayo mtoto wa kike anakuwa katika...
Mchimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Erick Peter (36) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari Tanzanite wa kidato cha nne.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Benjamin Kuzaga akizungumza leo...
Mbunge wa Viti Maalumu, Hawa Mwaifunga ameitaka Serikali kuongeza nguvu ya kutoa elimu kwa jamii ili kupunguza tatizo la mimba za utotoni huku akieleza moja ya sababu ni wanafunzi kufuata shule mbali na makazi yao.
Ametoa kauli hiyo alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya...
Great thinkers,
Hivi karibuni kumekua na ongezeko kubwa la mabinti wenye umri mdogo (umri Kati ya miaka 14-20s) kupata watoto. Nini kifanyike kumaliza hili tatizo?
Kanda ya ziwa, kumeibuka ubakaji wa watoto wa kike. Hali hii imekidhiri na ina usiri mkubwa na serikali ngazi mkoa, wilaya na kata zimepiga kimya. Rais sikiliza habari hii hapo ni shinyanga mjini, huko vijijini Hali Sio shwari
Mimba za utotoni kikwazo kwa mabinti wengi vijijini
Habari wanajamvi,
Naomba kuwasilisha kwenu andiko hili kuhusiana na changamoto ya mimba za utotoni.
UTANGULIZI
Tunapozungumzia mimba za utotoni tunamaanisha ni ile hali ya kuwa na ujauzito kwa binti yeyote ambae hajatimiza umri wa miaka 18...
Afisa Ustawi wa Jamii mkoani Morogoro, Jesca Kamugela amesema Matukio ya mimba na ndoa za utotoni yamezidi kuongezeka katika mkoa huo ambapo katika kipindi cha mwaka mmoja 2020/21 ya watoto 1,277 wamepata ujauzito kulingana na matukio yaliyoripotiwa.
Halmashauri zote za Morogoro zimekuwa...
Amina (siyo jina halisi)mwanafunzi wa kidato cha tatu katika mojawapo ya shule za sekondari wilayani Kibaha mkoa wa Pwani kila siku anaamka saa 11 ili awahi kwenda shule,shule iliyopo umbali wa kilometa sita kutoka nyumbani kwao.Kila siku anaenda na kurudi kwa miguu, nyumbani hapati kifungua...
Mwanafunzi anayesoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Uzogole Manispaa ya Shinyanga (jina limehifadhiwa), amedaiwa kujitoa ujauzito kwa kijichokonoa na kijiti, ili aendelee na masomo.
Imeelezwa mwanafunzi huyo alipata ujauzito huo wakati akiwa nyumbani akisubiri matokeo ya kidato cha...