Na Christian Bwaya
Ninapata chai ya jioni na Injinia. Jamaa kafanikiwa. Maisha yake yanaongea na kuhamasisha wengi. Jamaa anaheshimika na kanipa heshima ya kikao. Simu zimeachwa yatima mezani kwa takribani saa mbili zilizopita.
Injinia anaomba kutoka akateme mate kidogo. Namruhusu...