Mlima Kilimanjaro
Kilimanjaro ni jina la mlima mrefu kuliko yote barani Afrika. Mlima huo uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa mita 5,895 (futi 19,340).
Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi ya mlima tu, ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hiyo...