Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire, amesema kuwa hali ya maji katika Mto Ruvu ni ya kutosha, hivyo wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam wasiwe na hofu ya upungufu wa maji.
Mhandisi Bwire ameyasema hayo leo, Machi 11...