Habari za leo wana Jf. Naombeni msaada wa mawazo ya kumfanya mtoto wangu apende kula.
Mtoto wangu ni wakike anaumri wa miaka 5 sasa. Afya yake sio mbaya ila tatizo lake HAPENDI KULA.
Kila siku lazima nimshikie fimbo wakati wa kula. Nikulazimishana ni vilio mwanzo mwisho mpaka chakula kinaisha...