Kwa upande wangu kuna kipindi nilisafiri kwa siku kadhaa, nikiwa huko nikapigiwa simu kwamba wezi wamevunja dirisha ghetto kwangu na kuniibia. Ikabidi nikatishe shughuli zilizonipeleka kule na kuamua kurudi niangalie mazingira. Hawakuchukua vitu vyote, ila vilivyobaki navyo viliharibika...