Walipo ipata mali, wakaingia mjini
Wakamtupa jalali, jembe na wake mpini
Wakaponda zote mali, na warembo limbukeni
Wakachana daftari, kupoteza taarifa
Walikula na kusaza, wakaota na vitambi
Meza wakatandaza, kwa peza za rambi rambi
Rambi rambi zake faza, aliewaeleza kwamba
Kama mnataka mali...