nfra

No Wikipedia entry exists for this tag
  1. Mzee wa Code

    NFRA itulipe Wakulima wa Mbinga (Ruvuma) tuliouza Mahindi, ukimya wao ni maumivu kwetu

    Mimi ni Mkulima kutoka Mbinga mkoani Ruvuma, nimekuja mbele yenu nikiwa na changamoto ambayo kwa imani yangu najua kupitia nyie naweza kupata msaada ambao kimsingi sio tu utanisaidia pekee yangu bali sisi sote wenye hii changamoto. Naomba sauti hii ifike kwa Wizara ya Kilimo na ngazi ya juu ya...
  2. Frustration

    Miezi 3 inaelekea NFRA hawajalipa mahindi mkoa wa Ruvuma kwa wakulima. Pia kodi kwenye malipo kuna kodi mkulima anakatwa

    Habari za asubuhi Watanzania wenzangu. Kwenye nchi hii kuna mambo yanaenda hovyo sana toka utoaji wa taarifa,maandalizi na mfumo mzima wa NFRA kama wakala wa chakula nchini. Ikumbukwe wakala huyu alijinabaisha kuwa sasa atajiongezea jukumu lingine la kufanya biashara na wakulima wa mahindi...
  3. N

    DOKEZO NFRA inahujumu mfumo wa Stakabadhi Ghalani

    Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa, yaani NFRA ni Taasisi iliyoanzishwa mahsusi kuhakikisha kuna kuwepo na Hifadhi ya Mazao ya Chakula muda wote Nchini. Hununua mazao ya Chakula, kuyahifadhi, kuyachakata, kuweka kwenye Vifungashio na Hatimaye kuuza ndani na nje ya Nchi. Mazao ya Chakula...
  4. Clark boots

    NFRA wanachelewesha malipo ya mauzo ya mahindi kwa wakulima

    Ndugu Watanzania, ikimbukwe kuwa mwezi July serikali ilitangaza kununua Mahindi kwa wakulima kupitia wakala wa hifadhi ya chakula "NFRA" ila kitu kinachoshangaza na kustaajabisha ni kuwa malipo yanachelewa sana, wakulima wanakaa zaidi ya wiki tatu hali ya kuwa fedha zilishatengwa tayari...
  5. Fall Army Worm

    Utaratibu wa kuiuzia mahindi Serikali kupitia NFRA ni mgumu sana

    Wakuu habari za siku nyingi? Bila kupoteza muda ni kwamba tunaishukuru Serikali yetu kwa kutusaidia kupata soko la mahindi lakini tunalia na NFRA.Siku ya jumanne iliyopita,tarehe 24/07/2024; Nilipeleka mahindi yangu NFRA kituo cha Kakozi,mkoa wa Songwe. Nikaelekezwa kuwa niyachekeche...
  6. K

    Sheria ya kuruhusu National Food Reserve Agency (NFRA) kuagiza sukari toka nje ya nchi imekwisha sainiwa?

    Katika kikao cha Bunge kilichomalizika hivi karibuni walitunga sheria ya kuruhusu National Food Reserve Agency (NFRA) kuagiza sukari toka nje ya nchi. Je sheria hiyo imekwishasainiwa na Mhe. Rais?.
  7. Suley2019

    Hasunga: Mauti yalimkuta Milton Lupa wakati akienda kuripoti nafasi mpya

    Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga amesema kabla ya kifo cha aliyekuwa mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Milton Lupa kimetokea akiwa njiani kuripoti katika wadhifa mpya. Hasunga amesema alizungumza naye siku tatu kabla kuhusu uhamisho wake kutoka katika...
  8. Mkulima wa Maharage

    NFRA lipeni fedha za mahindi ya wakulima ili waanze maandalizi ya kununua pembejeo

    Tunaishukuru sana Serikali kwa uamuzi wa kununua Mahindi ya Wakulima kwa Bei elekezi ya KG 1 Tsh 860. Hata hivyo tangu Wakulima wapekele Mahindi yao bado hawajalipwa Fedha zao hali inayosababisha kuleta ugumu wa kufanta maandalizi ya Kilimo kwa msimu huu wa Masika ambao kwa mikoa ya Nyanda za...
  9. mtwa mkulu

    Sakata la kushuka kwa Bei ya Mahindi: Spika Tulia na Waziri Bashe wawataka wananchi wabebe mahindi yao wakauze NFRA

    Hatimaye spika tena ameonyesha ubabe kwa wabunge. Amewazuia wasiongee chochote kuhusu mahindi badala yake wawaelekeze wananchi wakajitwishe mahindi yao nakuuza huko NFRA ambako kuna bei nzuri. Hakika haya ni maafa mengine kwa Taifa letu. Wananchi vijijini ni masikini wa kutupwa lakini hawana...
  10. BARD AI

    Aliyemtumia Rais Samia taarifa za wizi wa Mahindi ya NFRA atafutwa na Polisi

    Jeshi la polisi wilayani Handeni mkoani Tanga linamsaka aliyetuma ujumbe kwa Rais Samia wa kuibiwa mahindi ya msaada ya NFRA kwa kutumia jina la Mwenyekiti wa kijiji. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe leo Desemba 30,2022 alipokuwa kwenye kikao na wananchi wa...
  11. Ojuolegbha

    CCM yatoa maelekezo kumaliza sintofahamu ununuzi wa mahindi Songea

    Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wakala wa chakula NFRA kuweka utaratibu mzuri ili kumaliza sintofahamu iliyopo juu ya ununuzi wa mahindi Manispaa ya Songea kwa kuhakikisha wananchi wote waliokwisha kuorodheshwa Mahindi yao yananunuliwa pamoja na kuongezwa kwa kituo kimoja cha ununuzi wa...
  12. ndenjii handsome

    Serikali fungueni mipaka wakulima wauze wenyewe mahindi, NFRA inawanufaisha wachache

    Baada ya kusikia serikali imetoa bilioni 50 kwa ajili ya manunuzi ya mahindi. Nikaona huu ndio wakati muafaka wa kuuza nikajaza howo zangu tatu mzigo kupeleka kwenye kitengo. Dah nilichokutana nacho tajiri atabaki kuwa tajiri nae maskini atazidi kuwa maskini hasa kwenye nchi zetu za Kiafrika...
  13. M

    Kassim Majaliwa: Serikali imetoaTsh. bilioni 15 kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kununua mahindi toka kwa wakulima

    Kupitia kwa WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeshatoa sh. bilioni 15 kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili kununua mahindi kutoka kwa wakulima. “Uzalishaji wa mahindi ni mkubwa lakini na sisi pia tumeimarisha hifadhi yetu ya Taifa ya chakula. NFRA tumeipa fedha za...
Back
Top Bottom