Uteuzi wa Dk Stergomena Tax kuwa mbunge, unaibua hisia kama ni mwanzo wa Rais Samia Suluhu Hassan kupangua Baraza la Mawaziri.
Dk Stergomena, mwanamke mwenye heshima kubwa kwenye uga wa kidiplomasia, anaingia bungeni kipindi ambacho Taifa halina Waziri wa Ulinzi kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa...