Katibu wa Baraza la Wazee wa Jiji la Arusha, Mzee Amimu Ngalawa, ameomba serikali kuongeza kiwango cha pensheni kwa wastaafu, akisema kiasi wanacholipwa ni kidogo na hakiendani na muda waliotumikia kulinganisha na marupurupu wanayopata wabunge baada ya kuhudumu kwa miaka mitano pekee...