Na Ahmed Rajab
PROFESA Mohamed Hassan Abdulaziz aliyefariki dunia jijini Nairobi asubuhi ya tarehe 10 Julai akiwa na umri wa miaka 91 alikuwa gwiji wa isimu, Kiswahili na Kiarabu. Zaidi ya hayo alikuwa msomi wa wasomi wenye kuhusika na mambo ya lugha na alikuwa mwalimu wa waalimu wa fani hiyo...