Kesi ya tuhuma za uporaji wa gari aina ya Range Rover, inayomkabili aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda na mmiliki wa blogu ya Lemutuz, William Malecela imepangwa kutajwa Desemba 8, 2022.
Ni baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate kuwa kwenye majukumu mengine ya kikazi...