Mlikubali wenyewe, bila mtutu kichwani,
Mkaazimu nipewe, kwa udi na kwa ubani,
Akasaini mwenyewe, kwa agizo la fulani,
Kama hamtaki ndoa, rudisheni pesa zangu.
Aliyeleta mzozo, ni mtoto mtukutu,
Akavujisha uozo, ukafika hadi Mbutu,
Wakatilia mkazo, wananzengo wenye utu,
Kama hamtaki ndoa...